Mgunduzi wa Madini ya
Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma, ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili, leo amenza matibabu katika Hospitali
ya Apollo jijini New Delhi nchini India.
Kwa mujibu wa binti
yake, Bi. Asha Ngoma, mgunduzi huyo ameamua kusaka matibabu zaidi baada ya kufanyiwa matibabu ili kuona kama
anaweza kupona kwa uharaka zaidi.
“Mzee amekuwa
akipatiwa matibabu tokea wakati ule Rais Magufuli alipomzawadia pesa shilingi milioni 100 mwezi
wa Aprili mwaka huu ya matibabu wakati uzinduzi wa ukuta unaozunguka machimbo ya
madini Mirerani mwezi April mwaka huu.
“Tunamshukur sana Rais
Magufuli kwani pesa hiyo tulipewa mara moja nasi tukaanza matibabu hapo
nyumbani na kwa kweli amemsaidia sana
sana na hapa India tunatarajia matibabu
yatamsaidia zaidi”, alisema Bi. Asha ambaye ameongozana na mjukuu wa Mzee Ngoma, Khalifa.
Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akipokewa na muuguzi leo tayari kupelekwa kuanza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. Pamoja naye ni bintiye, Asha Ngoma na mjukukuu, Khalifa
Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akiwa kwa daktari baada ya kupokelewa katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. Pamoja naye ni bintiye, Asha Ngoma na mjukukuu, Khalifa
Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akiingizwa wodini tayari kuanza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India.
Daktari wa zamu akimpima Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma mara tu baada ya kufikishwa wodini katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...