MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF)umekabidhi mifuko 245 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza inayojengwa eneo la Lusanga ambayo itaondoa changamoto ambazo walikuwa wakikumbana nazo wananchi.
Makabidhiano hayo yalifanyika juzi wilayani Muheza na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Ally Mwakababu kwa Mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Mwanasha Tumbo ambapo mifuko hiyo itasaidia ujenzi huo
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo wa saruji,Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha aliushukuru mfuko huo kwa kuona umuhimu kusaidia juhudi walizoanzishwa za ujenzi wa hospitali hiyo ili kuwapunguzia adha wananchi ikiwemo kuunga mkono jitihada za harambee iliyoendshwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu.
Alisema msaada huo umefika wakati muafaka wakiwa kwenye harakati za kuendelea na ujenzi wa hospitali hiyo ambao ni muhimu kwa ustawi wa wakazi wa wilaya hiyo katika kuhakikisha wanakuwa nayo ili iweze
kuwahudumia.
Mkuu huyo wa wilaya alisema ujenzi wa hospitali hiyo ambao utagharimu bilioni 11 mpaka itakapo kamilika lakini hatua iliyopo kwa harambee walioifanya Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu waliweze kupata bilioni 1.7.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...