Na Francis Godwin, Michuzi Blog, Iringa 

MFUKO  wa   hifadhi ya  jamii (NSSF)  umetoa  msaada  wa  mashuka 300 yenye  thamani ya  zaidi ya  shilingi  milioni 4.5  kwa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  na  halmashauri ya  Iringa mkoani  Iringa  kwa ajili ya  kusaidia hospitali  ,zahanati na  vituo  vya afya vyenye upungufu wa mashuka ya  wagonjwa.
Akikabidhi  msaada  huo  leo  meneja  wa  NSSF  mkoa  wa Iringa  Josephat  Komba  alisema  kuwa NSSF  imetoa msaada  huo  ikiwa ni  sehemu ya  utekelezaji  wa maombi yaliyotolewa na  Halmashauri  hizo  kwa  NSSF  kuomba  kusaidiwa msaada wa mashuka.
Komba  alisema kuwa NSSF  kama  mfuko  wa  hifadhi ya jamii  unayojukumu  la kuendelea  kuunga mkono  jitihada  za  Halmashauri  nchini  katika  kutoa  huduma  za  afya na  pia  unaendelea  kuunga  mkono   jitihada  za  serikali ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais Dkt  John Magufuli  kuona  sekta ya  afya  inaendelea  kuboreshwa  zaidi.
Kwani  alisema  NSSF pamoja  na majukumu mengine itaendelea  kuwa karibu na  jamii ya kitanzania kwani hatua  ya  waajiri kuwaunganisha  wafanyakazi wao na  NSSF  ni kutaka  kuona  maisha yao  yanaendelea  kuboreshwa  zaidi  hivyo  jukumu lao kuona  NSSF  inaendelea kuunga mkono azima ya  serikali katika  uboreshaji wa  huduma  za afya.

Meneja  wa NSSF  mkoa wa  Iringa Josephat  Komba(kushoto) akimkabidhi msaada wa  shuka  200  kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Omary  Mkangama  kwa  ajili ya  Hospitali ya  Frelimo 
 Wafanyakazi wa  hospitali ya  Frelimo wakitandika  mashuka  yaliyotolewa na  NSSF 
 Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Iringa Robert Masunya (kulia )  akishukuru kwa msaada wa  NSSF.
o 
Meneja  wa NSSF  mkoa wa  Iringa Josephat  Komba  (kushoto ) akimkabidhi msaada  wa mashuka  100 mkurugenzi wa  Halmashauri ya  Iringa Robert Masunya. Picha na Francis Godwin, Michuzi Blog, Iringa




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...