Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
Nusu fainali ya kwanza ya Fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi inatarajiwa kuchezwa leo kwa kuzikutanisha timu za Ubelgiji na Ufaransa.
Mchezo huo wa kwanza utakuwa ni muhimu kwa makocha wote wa timu mbili , Roberto Martinez wa Ubelgiji na Didier Deschamps wa Ufaransa.
Kwa upande wa Kocha wa Ufaransa Deschamps ameweka wazi mkakati wake wa kutaka kuweka rekodi ya kushinda taji hili akiwa meneja baada ya kuiongoza Ufaransa kushinda taji hilo mwaka 1998 akiwa nahodha wa kikosi cha dhahabu.
Deschamps atapambana na mchezaji mwenzie aliyekua katika kikosi hicho cha dhababu mwaka 1998 wakichukua ubingwa wa dunia Thiery Henry ambaye yupo kwenye benchi la ufundi la Timu ya Ubelgiji kwa sasa
Martinez kwa upande wake anaongoza kikosi chake ambacho kinatajwa kuwa na wachezaji wengi nyota katika historia ya soka la Ubelgiji.
Ubelgiji iliwaondoa Brazil katika hatua ya robo faainali kwa mabao 2-1 wakati Ufaransa iliinyuka Uruguay kwa mabao 2-0.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...