Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
PROPERTY International Limited imewahimiza watumishi wa umma na hasa walimu na wauguzi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya kujipatia viwanja kwa bei nafuu.
Tayari Property International Limted imesema kuanzia Julai mwaka jana wameuza viwanja kwa watumishi wa kada hizo wapatao 2000 lakini imeendelea kuwahimiza kuchangamkia fursa hiyo kupitia mradi maalumu wa viwanja ambao umetengwa kwa ajili yao.
Hayo yamesemwa na Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu wakati anazungumzia kuhusu miradi mbalimbali ya viwanja ambayo wanayo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kumiliki kiwanja ambacho kimepimwa na kilicho maeneo sahihi kwa makazi.
Akizungumza akiwa kwenye banda lao katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Maingu amesema kuwa wanayo miradi mingi ya “Tunawashauri walimu na wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya unafuu wa bei ya viwanja vyetu.Watapa viwanja kwa gharama nafuu kwani kuna punguzo la bei kwa ajili yao.
“Tangu tuanze kuuza viwanja kwa ajili ya watumishi hao kwa mkoa wa Dar es Salaam muamko umekuwa mkubwa kwani wengi wamenunua.“Hata hivyo tunaendelea kuwasisitiza walimu na wauguzi ambao bado hawajununua viwanja waje na tutazungumza nao, lengo letu ni kuona watumishi wetu wanakuwa kwenye makazi salama,”amefafanua.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Property International Tanzania Leila Maingu akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wakati akizungumza kuhusu uuzaji wa viwanja katika miradi mbalimbali hapa nchini kutoka Kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi akizungumza jambo na Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu katika banda la kampuni hiyo lililoko kwenye viwanja vya TANTRADE Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam ambapo maonyesho ya biashara ya Sabasaba yanaendelea
Mmoja wa wafanyakazi akiwahudumia wananchi waliotembelea katika banda hilo.
Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu paoja na wafanyakazi wenzake wakiwahudumia wananchi mbalimbali waliofika kwenye banda hilo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...