*Atoa maagizo kuhakikisha gawio linaendelea kuongezeka
*Awaambia Serikali yake haipendi shirika bali inapenda pesa
*Wasiotoa gawio awataka waone aibu, kisha wajitathamini
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
RAIS Dk.John Magufuli amepokea gawio la Sh.bilioni 723 kutoka kwa kampuni na taasisi mbalimbali huku akieleza wale ambao hawajawahi kutoa gawio menejimenti yake ijitathimini na ione aibu.
Pia amesema kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Serikali umeufanya bado gawio hilo halitoshi na hivyo ameomba mamlaka husika kuhakikisha zinasimamia kampuni na mashirika hayo ili kuongeza gawio kwa serikali.
Kampuni mbalimbali ikiwamo Kampuni ya mafuta Puma Energy ambayo nayo nimiongoni mwa walitoa gawio kwa kuipa Sh.bilioni 9.Utoaji huo wa Gawio umefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais Magufuli amepongeza kampuni na taasisi zote ambazo zimetoa gawio nakueleza kwamba kuna baadhi ya kampuni tangu nchi kupata uhuru hazijawahi kutoa gawio.
“Tukio la kupokea fedha hizi za gawio Sh.bilioni 723 ni tukio muhimu katika nchi yetu kwani fedha hizi ndizo ambazo zinatumika kufanya maendeleo,”amesema Rais Magufuli na kuongeza Serikali haipendi shirika bali inapenda fedha, hivyo ambao hawajatoa na wenyewe watoe.
Pia amefafanua duniani kote kuna njia mbili za kupata mapato, njia ya kwanza ni kwa makusanyako ya kodi na njia ya pili ni ile ambayo haitokani na makusanyo ya kodi ikiwamo hiyo ya gawio. “Kwa njia moja au nyingine Serikali imejitahidi kuimarisha ukusanyaji wa kodi ambapo Mwaka wa fedha wa 2016/2017 wamekusanya Sh.Trilion 15.5 .
“Wananchi kutokana na mambo ya maendeleo yanayofanyika wamehamasika katika kulipa kodi na ndio maana makusanyo yameongezeka,”amesema Rais Magufuli. Wakati huohuo amesema kuna mashirika zaidi ya 90 yanayostahili kutoa gawio kwa Serikali lakini kampuni ambazo zimetoa ni 47 tu.Amesema mwaka 2016 mashirika 25 yalitoa gawio na hata hivyo gawio hilo halikuridhisha Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bw. Edwin Rutageruka. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...