Hyasinta Kissima- Afisa Habari Halmashauri ya Mji Njombe

Halmashauri ya Mji Njombe imepokea jumla ya pikipiki 13 zenye thamani ya shilingi milioni 39 kwa waratibu elimu Kata 13 lengo ikiwa ni kufanya ufatiliaji na usimamizi wa elimu katika Kata.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Salum Mkuya amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuboresha sekta ya elimu kwa kuhakikisha kuwa wasimamizi wa elimu wanawezeshwa upatikanaji wa vitendea kazi ili kufanya mazingira ya kazi kuwa rafiki.

“Pikipiki hizi zikafanye kazi ya ufuatiliaji kwa kupandisha kiwango cha ufaulu, kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma na kuandika ikiwa ni sambamba na kuthibiti utoro mashuleni.”Alisema Mkuya.Aidha, Mkuya ameiomba Halmashauri kuhakikisha kuwa pikipiki zote zilizokabidhiwa zinapatiwa bima kama serikali ilivyoagiza.

Naye mwenyekiti wa Halmashauri Edwin Mwanzinga amesema kuwa anaishukuru serikali ya CCM kupitia kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kutambua umuhimu wa pikipiki hizo kwa waratibu elimu kwani itarahisisha shughuli za usimamizi na ufuatiliaji elimu hususani katika Halmashauri ambazo maeneo mengi jiografia yake ni ngumu kufikika kutokana na ukubwa wa eneo halikadhalika changamoto za miundombinu.

“Najua waratibu mlikua mnafanya kazi katika mazingira magumu niwaombe sasa tukafanye kazi bila visingizio na ni lazima tuwe wa kwanza kimkoa kwa sababu tumepata vitendea kazi. Lakini niwaombe sana mkazitunze pikipiki hizi ili tuweze kwenda nazo kwa muda mrefu. Kwa wale ambao hamjui kuzitumia tusitumie pikipiki hizi kujifunzia. Ni imani yangu mtaenda kujifunza mpate leseni na muweze kuzitumia vizuri na kwa tahadhari” Mwanzinga alisema

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waratibu elimu Ester Mjuu Mratibu Elimu Kata ya Ramadhani Halmashauri ya Njombe alisema kuwa sasa wataweza kufika kila kona ya Kata zao katika kufuatilia usimamizi wa elimu.“Tunashukuru sana kwa vitendea kazi hivi,miongoni mwa changamoto iliyokuwa inatukabili imepata ufumbuzi tutaenda kufanya kazi kwa kadri mlivyotuelekeza ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na Taifa la wasomi kwa kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa karibu kwenye sekta ya elimu.”Alisema
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Salum Mkuya akikabidhi Pikipiki kwa ajili ya waratibu elimu Kata 13 kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga akitoa mkono wa pongezi kwa Mratibu Elimu Kata ya Ramadhan Ester Mjuu mara baada ya kumkabidhi pikipiki.
Waratibu Elimu Kata kutoka Katika Kata 13 za Halmashauri ya Mji Njombe wakipongeza serikali kwa jitihada za kuwapatia Pikipiki ikiwa kama nyenzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...