Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kujenga miundo mbinu ya barabara hasa za ndani kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kuyafikia masoko.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. “Serikali imetoa shilingi bilioni 6 kujenga barabara ya Rujewa – Ubaruku inajengwa kwa kiwango cha lami”

Makamu wa Rais ameipongeza kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd kwa kujenga kituo cha afya kitakacho hudumia watu zaidi ya elfu kumi na kulaza wagonjwa 42 kwa wakati mmoja. Aidha Makamu wa Rais amesema migogoro yote itafanyiwa kazi kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mmoja.

Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mhe. Haroon Pirmohamed ameahidi kuwalipia deni la shilingi milioni 800 wakulima wanaodaiwa deni waliokupa kununulia power tila .Mbunge huyo wa Mbarali amesema kuwa Serikali ya awamu imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.

Akizungumza na Wananchi wa Kapanga katika mkutano huo, Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ameahidi kutoa mifuko 200 kutoka kwenye Taasisi yake ya Tulia Trust kusaidia ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika kituo cha Kapanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mchele unaozalishwa na kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd , kulia ni Mkuu wa kampuni hiyo nchini Bw. Nillard Chawdry akimpa maelezo Makamu wa Rais namna wanavyotumia teknolojia ya kisasa katika kukoboa na kufungasha mpunga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akihutubia wananchi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Kapunga,pichani kushoto ni Mkuu wa kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd Bw. Nillard Chawdry.Kituo hicho kimejengwa na Kapunga Rice Project Ltd kitakacho hudumia watu zaidi ya elfu 10 na kulaza wagonjwa 42 kwa wakati mmoja. Kituo cha Afya Kapunga ambapo Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi .Sehemu ya Wakazi wa kijiji cha Kapunga waliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...