Na Lorietha Laurence-WHUSM,Mbulu Mjini
Serikali imeandaa mpango wa kuwaenzi watu mashughuri wakiemo wanamichezo wakongwe ambao wamewahi kuliletea taifa heshima katika mashindano mbalimbali akiwemo mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari.
Hayo yamesemwa leo Mbulu Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipomtembelea mwanariadha huyo nyumbani kwake ambapo alipata fursa ya kuona medani , tuzo na vikombe alivyowahi kushinda mwanariadha huyo.
“ Sisi kama Wizara tumeanzisha kampeni ya Uzalendo ambapo mwaka jana tuliwaenzi wasanii wa zamani wa muziki na mwaka huu mnamo Oktoba 14 ni zamu ya wanamichezo wakongwe akiwemo Bw. John Akwhari ” amesema Mhe. Shonza .Alizidi kueleza kuwa amevutiwa na jinsi mwanariadha huyo anavyotunza kumbukumbu zake huku akiwataka wanamichezo na watu wengine kuiga mfano huo bora ili kuviwezesha vizazi vijavyo kupata historia nzuri katika sekta ya michezo.
Naye Mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari amesema amefurahi kuona Serikali inatambua na kuthamini mchango wake katika sekta ya michezo na kuhaadi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kwa pamoja kuleta maendeleo katika sekkta hiyo muhimu.
Bw.
John Akwhari ni mwanariadha wa zamani wa Tanzania wa kwanza kufungua
milango ya kushiriki riadha nje ya nchi ambapo alijizolea umaarufu
katika mashindano ya mwaka 1968 ya Olimpiki nchini Mexico ambapo licha
ya kuwa wa mwisho aliueleza umati kuwa nchi yake ilimtuma kumaliza mbio
na siyo kuanza mbio.
Naibu
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
(Kushoto) akiangalia vikombe vya ushindi
alivyowahi kushinda Mwanariadha Mkongwe Bw. John Akwhari (Kulia) alipofanya
ziara ya kutembelea nyumbani kwake Mjini Mbulu hapo Jana.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...