Na Frankius Cleophace, Tarime

SERIKALI imetoa Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha Afya katika kata ya Nkende Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kwa lengo la kusogeza huduma ya afya karibu na Wananchi.

Huku wananchi hao wakichangia kununua eneo lenye thamani ya Sh.milioni 8 kwa lengo la upanuzi wa eneo hilo ili kuweza kufanikisha mchakato huo. 

Akizungumzia ujenzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime Elias Ntiruhungwa amesema kuwa tayari Serikali imeshapelekal kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Nkende.

“Mpaka nazungumza kwa sasa hivi tayari fedha zipo kwenye akaunti na hivyo nataka kuona wiki hii kila kitu kimekamilika na ujenzi kuanza mara moja leo nimeambatana na wataalamu wote ili kumaliza mapema shughuli hii,” amesema Elias.Pia Elias amewapongeza wananchi kujitoa kununua eneo kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa kituo cha Afya na kuahidi kuendelea kushirikiana nao vyema ili kumaliza mapema ujenzi huop.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote amesema kuwa wananchi wamewiwa ujio wa ujenzi wa kituo cha afya na ndo maana wamejitoa kwa nguvu zao ili maeneo ya kutosha yapatikane huku akishukuru Serikali kutoa Fedha hizo.

“Nimeweza kushawishi wananchi wangu kuchangia na mimi nikiwa wakwanza kuchangia ili tununue eneo la kutosha ata kama halitatosha bado kunaeneo lingine takribani heka tisa bado tutapendekeza eneo hilo ili kujenga Kituo cha afya kwa lengo la kunusuru Wananchi ambao ulazimika kwenda katika hospitali ya Wilaya ya Tarime,” amesema Komote.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na Wakazi wa kata ya Nkende katika mtaa wa Magena ambapo wanatarajia kujenga kituo cha Afya baada ya Serikali kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 400.
Zahanati ya Mtaa wa Magena ambayo inahudumia wakazi wa kata ya Nkende Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote akiongea na Wananchi katika eneo la mtaa wa Magena ambapo wanatarajia kujenga kituo cha Afya.
Jengo linalomilikiwa na Ccm tawi la Magena ambalo wametoa eneo hilo lenye thamini ya Millioni 10 ili kujenga Kituo cha Afya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...