Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkoa wa Simiyu umepokea jumla ya vitabu 174,188 awamu ya kwanza kwa masomo ya Kiingereza na Hisabati, vyenye thamani ya takribani shilingi milioni 348 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne, ambavyo ni sawa na uwiano wa mwanafunzi mmoja kwa kitabu kimoja.
Akizungumza na viongozi , baadhi ya walimu na wanafunzi wa mkoa wa Simiyu kabla ya kukabidhi vitabu vitabu hivyo kwa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Julai 05 jioni mjini Bariadi, Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini, amesema Taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha vifaa vyote vya kielimu ikiwemo vitabu, vifaa vya maabara na vifaa vingine vinavyohitajika vinapatikana.
Amesema utoaji wa vitabu 29,003 kwa kila somo kwa wanafunzi wa darasa la nne Mkoani Simiyu ni sehemu ya utekelezaji wa elimu bila malipo, huku akibainisha kuwa Taasisi ya Elimu inatarajia kuzalisha vitabu 681, 527 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne nchi nzima.
Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema wamepokea vitabu awamu ya kwanza kwa masomo ya kiingereza na hisabati kwa uwiano wa kitabu kimoja mwanafunzi mmoja, huku akibainisha kuwa vitabu vilivyobaki vinatarajiwa kuletwa tena wiki ya kuanzia tarehe 16 Julai, 2018 na akawataka walimu na wanafunzi kuvitumia vitabu hivyo kama ilivyokusudiwa.
“Naishukuru sana Serikali kwa kutoa vitabu hivi hadi sasa tuna wanafunzi 53, 187 darasa wa nne na vitabu tulivyopokea kwa awamu hii kwa masomo ya Hisabati na Kiingereza, kila mwanafunzi wa Mkoa wa Simiyu atapata kitabu cha kwake, kwa masomo manne yanayobaki tumeahidiwa kuwa baada ya majuma mawili vitakuwa vimefika” alisema Afisa Elimu Mkoa.
Kwa upande wao wanafunzi wa mkoa wa Simiyu wameishukuru Serikali kwa kuwaletea vitabu, hivyo ambavyo wanaamini vitawasaidia kujisomea na kuinua ufaulu hatimaye kuufikisha mkoa huo katika mikoa kumi bora inayofanya vizuri kitaaluma.“Tunaishukuru sana Serikali kwa kuwaleta hivi vitabu, tunaamini vitawasaidia wadogo zetu wa darasa la nne kujifunza na kuongeza ufaulu na siku moja mkoa wetu na sisi utakuwa kati ya mikoa bora inayofanya vizuri kitaaluma “ alisema Liku Malisha mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Somanda A.

Mwakilishi
wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini(kulia) akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwa na baadhi ya viongozi
na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A vitabu vya Darasa la nne
mkoani humo, makabidhiano hayo yalifanyika Julai 05, 2018 katika Viwanja
vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akihojiwa
na waandishi wa habari baada ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka
Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne na Mwakilishi wa Taasisi ya
Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini, katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi Julai 05, 2018.
Mbunge wa Itilima Mkoani Simiyu, Mhe. Njalu Silanga akihojiwa na
waandishi wa habari baada ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Mtaka
kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu
Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini, katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi Julai 05, 2018.
Abdallah
Twalib Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda A,
akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne mkoani
humo na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini, katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi.
KUSOMA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...