Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kimesema kuwa idadi ya wanaojiunga katika Taasisi hiyo imekuwa ikiongezeka kila mwaka wa masomo kutokana na usimamiaji wa misingi ya taaluma wanayoitoa.

Akizungumza katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  (Sabasaba), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Taasisi hiyo, Gorah Abdallah amesema kuongezeka kwa idadi hiyo kunailazimu taasisi kuongeza  miundombinu ya majengo ili  kuendana na mahitaji yaliyopo.

Amesema moja ya mafanikio ya Taasisi hiyo ni wahitimu kupata kazi moja kwa moja kutokana na kuwa na taaluma bora ya kutumika  na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.

Abdallah amesema wameweka mpango mkakati wa miaka mitano unaoanzia 2019/23 ikiwa moja ya mkakati huo ni kufanya utafiti kwa wajasiriamali waliopo nchini ili kurasimisha ujasiriamali huo.

Aidha amesema kuwa wahitimu katika taasisi hiyo  ni kuwa na taaluma ya ujasirimali katika kupunguza changamoto ya ajira.

Amesema Taasisi hiyo inakwenda na mitaala ya kimataifa ili waweze kufanya kazi kwa weledi.

Gorah amesema kuwa wamejenga jengo la ghorofa saba litalochukua wanafunzi 3500 kwa wakati mmoja ambalo linatarajia kumalizika Septemba 2018 na ujenzi wa Kampasi ya Mtwara umeshakamilika na wako katika maandalizi ya kuhamia katika majengo yao na kuachana kupanga.

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TIA , Gorah Abdallah akizungumza katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 Baadhi wa watendaji waliopo katika banda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
 Afisa wa Idara ya Bajeti ya Serikali, Asajile Mwaipopo akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Idara ya Bajeti ya Serikali, Boniface Kilindimo
Ofisa wa Idara ya Bajeti ya Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Boniface Kilindimo akitoa ufafanuzi kuhusiana na bajeti inavyopangwa kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya  Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Kushoto ni Afisa wa Idara ya Bajeti ya Serikali, Asajile Mwaipopo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...