Na Dixon Busagaga wa Globu
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya abiria ukiwemo kuendesha bila leseni, umri wa kuendesha gari kupitiliza huku wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao.
Katika kituo Kikuu cha mabasi ya abiria yaendayo mikoani na yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu Operesheni kikosi cha usalama barabarani Inspekta Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi wa magari zaidi ya 800 ambapo yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku baadhi ya Madereva wakikutwa na silaha katika magari yao vikiwemo visu.
Kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .
Kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .
Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani Inspekta wa polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la kupunguza ajali huku baadhi ya Madereva na wananchi wakipongeza utaratibu huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Hamis Issah akimuuliza mmoja wa madereva waliokamatwa juu ya matumizi ya silaha ya Kisu kilichokutwa katika gari lake.



Dereva anayeendesha gari la abiria bila liseni akifanya ajali na kuua mtuu hukumiwe kama ameua kwa makusudi. Atiwe kamba.
ReplyDelete