
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christina Mndeme (akikagua tumbaku pichani) amefungua soko la ununuzi wa zao la Tumbaku katika kijiji cha Suruti Wilayani Namtumbo.
Katika ufunguzi huo, Mhe Mndeme amewaasa wakulima kufuata mbinu bora za kilimo zinazotolea na Maafisa ugani na kuacha tabia ya kuchanganya tumbaku , maji na mafuta kwa lengo la kuongeza uzito.
Mhe Mndeme ameonya Kufanya hivyo ni kosa kwani inaharibu soko la zao ambapo amekitaka chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU kusambaza pembejeo kwa wakati ili wakulima waweze kuzitumia kulingana na msimu wa Kilimo.
Akihitimisha Hotuba Yake Mhe Mndeme amewataka Wadau wote kutoa ushirikiano kwa wanunuzi wa tumbaku ili biashara iwe endelevu kwa manufaa ya Taifa, na mwananchi aweze kujikomboa kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...