Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza na Maafisa wa Ofisi ya Bunge alipotembelea Banda lao katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Eng. Stella Manyanya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Eng. Stella Manyanya na Maafisa wa Ofisi ya Bunge alipotembelea Banda lao katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi akisikiliza maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za Bunge kutoka kwa Mwandishi Mwandamizi wa Taarifa Rasmi za Bunge Bw. Paston Sobha alipotembelea Banda lao katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali Mirisho Sarakikya akisikiliza maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za Bunge kutoka kwa Mwandishi Mwandamizi wa Taarifa Rasmi za Bunge Bw. Paston Sobha alipotembelea Banda lao katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Bunge katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.
PICHA NA BUNGE







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...