Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Silvester
Mabumba amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za kibiashara
nchini Comoro kwani mazingira ya kibiashara nchini humo ni mazuri sana.
Mabumba amesema kwamba Visiwa vya Comoro hutegemea nchi ya Tanzania
kuagiza mahitaji yake yote ya msingi kama chakula, saruji, mbogamboga na vifaa vya
kiwandani, haswa fenicha. Amesema hata kijiografia, Visiwa vya Comoro ndio vilivyo karibu zaidi na hutegemea
Tanzania pekee kufanya nao biashara. Amesema biashara kati nchini zote mbili kwasasa
imekuwa hadi kufikia Tsh500 bilioni.
“napenda kuchukua fursa hii, niwasihi wafanyabiashara wa Tanzania, watumie nafasi hii
ya kipekee kwani Visiwa vya Comoro hutegemea kuagiza mahitaji yao yote ya chakula
na bidhaa nyingine kutoka Tanzania pekee,” amesema Mhe. Balozi Mabumba.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kwa upande wao
kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wamejipanga kushirikiana na
wadau kutatua changamoto zote zinazojitokeza kwa wafanyabiashara hao. Mhandisi Kakoko amesema kwamba TPA, kama muwezeshaji amejipanga kutoa
huduma bora na kwa ufanisi mkubwa ili kukuza biashara kati ya nchi hizo na kusaidia
kuongeza pato kwa TPA na serikali zote mbili kwa ujumla.
“huduma zikiwa bora na za haraka bandarini, huleta nafuu kwa mlaji na kuongeza
mapato ya serikali, hivyo sisi kama bandari ziara hii kwetu imekuwa ya mafanikio
makubwa kwani nimepata mambo ya kwenda kufanyia kazi zaidi ya niliyoyatarajia,”
amesema Mhandisi Kakoko.
Mhandisi Kakoko amesema kwamba kwa kushirikiana na wenzo wa Comoro wataanza
kwa kuboresha masuala ya kiusalama ambapo amesema kwamba watahakikisha kila
meli au boti inayochukua bidhaa Tanzania kwenda Comoro inatumia radio maalumu za
mawasiliano majini. Mbali na hilo amesema kwamba atahakikisha makubaliano yaliyofikiwa kati cha Moroco
Chamber of Commerce na Tanzania Chamber of Commerce ya Mtwara yanatekelezwa ili
kuboresha shughuli za ufanyaji biashara.
Mkurugenzi mkuu huyo wa TPA, pia aliahidi kuwasiliana na wenzao wa Zanzibar kuona
jinsi meli zao mbili zinavyoweza kusaidia kusafirisha mizigo kati ya nchi hizo kwani ni
salama zaidi na vumulivu. Visiwa vya Ngazidja na Anjouani ambavyo ndio vikubwa nchini Comoro kutegemea
Tanzania kuagiza mahitaji yake yote ya msingi haswa chakula kwa asilimia 70. Comoro huagiza zaidi mchele na viazi, mbogamboga, saruji na bidhaa nyinginezo za
viwandani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...