
Na Benny Kisaka
Marehemu Profesa Maji Marefu alikuwa rafiki sana wa wanahabari, ambapo alikuwa mstari wa mbele katika kuwa karibu nao katika shida na raha.
Mfano mmojawapo ni mwezi Novemba mwaka 2003 ambapo baada ya kukawama kiuchumi marehemu alijitolea kudhamini safari ya kwenda Nairobi, kuripoti mchezo kati ya Taifa Stars na Kenya kwa kutoa usafiri, chakula na malazi. Hakusita kufanya hayo mara tu baada ya kuombwa.
Katika picha hii Profesa Maji Marefu (mwenye kibandiko mstari wa mbele) anaonekana akiwa na baadhi ya waandishi hao katika hoteli ya Safari Park jijini Nairobi ambako Stars walifikia wakiwa chini ya kiongozi wa msafara katibu wa kamati ya Muda ya FAT( sasa TFF) wakati huo Mwina Mohamed Seif Kaduguda.
Wanahabari hao ni Masoud Sanani, Aboubakar Liongo, Benny Kisaka, Ibrahim Bakari, Eric Anthony, Peter Mwenda, Oscar Mbuza, Somoe Ng'itu, Mashaka Mhando, Ezekiel Malongo, Jesse John, Michael Maluwe, Ndembeju na Emmanuel Muga (sasa wakili msomi).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...