Kampuni ya usambazaji ya Pembejeo ya PETROBENA EAST AFRICA LTD imeanza kuunga mkono kwa vitendo Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungwano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha wanafikisha pembejeo za kilimo kwa wakati kwa wakulima nchini.
Akiongea leo mkoani Morogoro katika mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kwa maafisa kilimo na wasambazaji wa pembejeo,Mkurugenzi wa Kampuni ya PETROBENA Peter Kumalilwa amesema wameamua kuweka Ghala kubwa mkoani Morogoro ili kuhakikisha wakulima wa mkoa huo na mikoa jirani wanapata pembejeo kwa haraka kupitia wauzaji wadogo na wakubwa.
Kumalilwa amesema PETROBENA ikiwa wakala mkuu wa kampuni ya Mbolea ya YARA watahakikisha mbolea inapatikana katika katika kipindi chote na siyo kama ilivyo sasa katika maeneo mengi ambapo mbolea inaanza kupelekwa wakati wa msimu hali inayosababisha kuchelewa kutokana na ubovu wa miundo mbinu pamoja na umbali wa walipo wahitaji.
Ameongeza kuwa katika mkoa wa Morogoro wanatarajia kuwa na wauzaji wa pembejeo wapatao 700 katika wilaya zote sita ambao watapewa mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo itakayowasaidia kuwapa elimu wakulima wa mazao mbali mbali mkoani humo wakiwemo wa Miwa,Mpunga,Mahindi,Mboga mboga na mazao mengine.
Naye Afisa Biashara wa kampuni ya YARA nyanda za juu kusini John Meshak amesema wameamua kuzindua ghala la mbolea Morogoro kwa kuwa kuna wakulima wengi wanaolima mazao mengi ila hawapati nafasi ya kupata mbolea bora na kwa wakati hali inayopunguza kasi ya uzalishaji wa mazao yao.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya PETROBENA EAST AFRICA LIMITED Peter Kumalilwa mipango ya kampuni hiyo katika kumkwamua mkulima wa Tanzania.
Mtaalamu wa kilimo kutoka kampuni ya YARA Maulid Mkima akitoa darasa la kwa maafisa kilimo na maafisa wa pembejeo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi mpya ya PETROBENA mkoani Morogoro.Picha zote na William Bundala.
Maafisa Kilimo na Wauzaji wa Pembejeo kutoka wilaya za mkoa wa Morogoro wakiwa makini katika mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo na umuhimu wa kutumia mbolea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...