Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa washiriki wa mashindano ya urembo nchini kuzingatia maadili na tamaduni za kitanzania kwa kuwa kielelezo bora kwa jamii .
Hayo ameyasema jana Jijini Arusha wakati wa shindano la kumtafuta mrembwende wa Jiji hilo , yaliyoandaliwa na The Function House chini ya uongozi wa Mkurugenzi Bw. Tilly Chizenga yaliyoshirikisha warembo 19.
“ Ninyi ni kioo cha jamii, mnaangaliwa na jamii nzima hivyo msibweteke mnapopata umaarufu bali muwe kielelezo bora cha utamaduni na maadili ya Kitanzania ” amesema Mhe. Juliana Shonza . Anazidi kufafanua kuwa sanaa ya urembo ni ajira kama zilivyo ajira nyingine,na kuwaomba wazazi na jamii kutoa ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha mabinti wanatimiza ndoto zao katika sanaa hiyo.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Jiji la Arusha, shughuli iliyoandaliwa na The Fuction House chini ya Mkurugenzi Bw. Tilly Chizenga jana Jijini hapo.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Katikati) akifuatilia matukio mabalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na washiriki wa urembo waliokuwa wanawania taji la Miss Arusha, jana katika ukumbi wa Lake Nyasa AICC, kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Bw. Kalisti Lazaro na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa The Fuction House Mrs. Chizenga.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (mwenye gauni la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa taji la Miss Arusha baada ya kumalizika kwa mashindano hayo jana Jijini hapo . Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...