Watoto watatu kati ya tisa wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo waliokwenda kutibiwa  nchini Israel tarehe 28/5/2018 wanatarajiwa kurudi nchini leo. Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto  waliambatana na  wauguzi pamoja na wazazi wao. 

Watoto hao wamefanyiwa upasuaji wa moyo na hali  zao zinaendelea vizuri.  Watoto sita waliobaki wanaendelea na matibabu na watarudi nchini pindi afya zao zitakapoimarika. 

 Safari hiyo ya matibabu nchini Israel iliwahusu watoto wenye umri wa miezi tisa  hadi miaka 14 imeratibiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s  Heart – SACH) ya nchini humo. 

 Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) inatibu magonjwa mengi ya moyo (kwa asilimia 90) kwa watoto  kupitia  wataalamu wazalendo walionao. Hata hivyo wanamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache ambao ni asilimia 10 wanaohitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi kuliko uliopo hapa nchini kwa sasa na ushirikiano ni mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. 

Aidha JKCI ina madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita   na wauguzi wanne ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi hiyo. Daktari mmoja na wauguzi wawili bado wanaendelea na masomo nchini humo na hiyo itasaidia kwa siku za mbeleni zaidi ya asalimia 95 ya watoto watatibiwa  hapa nchini. 

Wakati huohuo watoto wengine wawili wanatarajiwa kuondoka leo jioni tarehe 11/7/2018 kwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu. Watoto hawa wataambatana na wazazi wao.

 Hili ni kundi la saba la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH)  wa kuwapeleka wagonjwa nchini humo.  Hadi sasa watoto 59 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo  ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

 Kwa wakinamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo au la. Kupitia kipimo hiki  mtoto akigundulika kuwa  na tatizo la moyo ataweza kupatiwa  matibabu kwa wakati  na hivyo kuwa na afya njema kama watoto wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...