Na Daniel Mwambene, Afisa Habari Ileje
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wameonywa dhidi ya matumizi
onyo hilo,lilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Haji Mnasi alipokuwa akizungumza na watumishi wake katika ukumbi wa Sekondari ya Ileje wakati wa kikao kazi alichokuwa ameitisha kwa Kata za Isongole na Itumba. mabaya ya mitandao ya kijamii ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuwakumba.
Mnasi alisema watumishi hawana budi kujiunga katika makundi mbalimbali ya kimitandao ikiwa ni haki yao ya msingi katika kutoa na kupata taarifa mbalimbali katika kidjitali lakini pia waangalie sheria za kimtandao ili kujiweka salama siku zote.
“Kuna watu wamekuwa wakipokea na kusambaza taarifa bila kutafakari,zikiwemo taarifa ambazo hazistahili kusambazwa kisheria hii ni hatari kwa ajira zenu mkizingatia kuwa wote tu watekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala (CCM)” alisisitiza kiongozi huyo.
Aliongeza kuwa ndani ya Halmashauri yake kuna makundi kadhaa ya ‘Whatsapp’ ambayo yameundwa ili kuwezesha watumishi kupashana habari za kimaendeleo na si kukebehi serikali iliyopo madarakani akisema kuwa atakayefanya hivyo atabeba mzigo wake mwenyewe.
Onyo hilo linakuja wakati Mamlaka ya Mawasiliano hapa nchini (TCRA) ikiendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mtandao ambapo sheria mpya zilishapitishwa ikiwa ni hatua mojawapo ya kuimarisha utaifa uliojengwa kwa muda mrefu unaoweza kuhatarishwa kupitia matumizi mabaya ya vyombo vya mawasiliano kama redio zilivyotumika vibaya wakati wa mauaji ya halaiki kule Rwanda na Burundi
Kwa upande wao watumishi hao waliiomba serikali kutuma taarifa kwa walengwa kwa wakati ili kuharakisha utekelezaji.
Bw. Herman Shola ambaye ni mwalimu wa Sekondari ya Itumba alisema kuwa kuchelewa kwa taarifa kufika kwa wakati hunachangia hata uchelewevu kwenye vikao.
Pamoja na mambo mengine watumishi hao toka kada mbalimbali ngazi ya wilaya hadi kijiji walikumbushwa wajibu wao utakampatia mwananchi huduma bora na kwa wakati. Aidha watumishi hao walimweleza mwajiri wao juu ya kero mbalimbali zinazopunguza ari ya kufanya kazi yakiwemo malipo ya likizo na kuchelewa kupanda kwa madaraja kwa mujibu wa sheri za Utumishi wa Umma. Vikao hivi ni mwendelezo wa vikao vinavyoendelea wilayani humo ikiwemo mikutano ya hadhara inayolenga kupunguza kero za wananchi na watumishi ili waweze kufurahia kuishi ndani ya wilaya hii.
![]() |
DED wa Ileje Ndg.Haji Mnasi(aliyesimama) akizungumza na watumishi wa Kata za Itumba na Isongole kwenye ukumbi wa Sekondari ya Ileje wakati wa kikao kazi alichoitisha |

Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wiya ya Ileje toka Ofisi ya DED NA Kata za Itumba na Isongole wakimsikiliza Mkurugenzi wao Ndugu Haji Mnasi
![]() |
Mwalimu Zayumba Gabriel wa Sekondari ya Itumba (aliyesimama)akitoa kero yake kuhusu malipo ya likizo. |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...