.
Muonekano wa Maporomoko ya Nkondwe jana ambayo ni moja ya kivutio cha utalii, katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu Maporomoko ya Nkondwe na fursa za utalii zinazopatikana katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi jana. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Salehe Mbwana Mhando.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wakifurahia maporomoko ya Nkondwe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya asili mkoani humo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia maumbo ya asili kwenye miamba iliyopo karibu na Maporomoko ya Nkondwe ambayo ni miongoni mwa kivutio cha utalii katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Salehe Mhando.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Tanganyika akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo, Selehe Mhando (kulia kwake) wakiwa wamepumzika kidogo baada ya kupanda mlima uliopo ndani ya Msitu wa Hifadhi wa North East Ugala baada ya kutembelea maporomo ya Nkondwe jana.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...