Na Hamza Temba, Rukwa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewasimamisha kazi Maofisa na Askari Wanyamapori wote 27 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA katika Pori la Akiba Uwanda akiwemo Kaimu Meneja, Lackson Mwamezi kwa kushindwa kusimamia vizuri pori hilo na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku tatu tangu amsimamishe kazi meneja wa Pori hilo, Mark Chuwa kwa tuhuma kama hizo pamoja na tuhuma nyingine ikiwemo kushindwa kuondoa ngo'mbe zaidi ya 12,000 ambao wamedaiwa kuwepo ndani ya pori hilo.
Pori la Akiba Uwanda lipo katika bonde la ziwa Rukwa katika wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na linasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Dk. Kigwangalla amefanya uamuzi huo jana alipotembelea pori hilo sambamba na kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kilyamatundu ambapo alipokea taarifa ya malalamiko kuhusu askari hao kupokea rushwa kutoka kwa watu wenye uwezo na kuwaruhusu kuchunga hifadhini huku wakiwanyanyasa masikini kwa kukamata mifugo yao.
Alifafanua tuhuma hizo kuwa ni pamoja na kudaiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wavuvi wanaovua samaki Ziwa Rukwa kwa kuwatozwa kila mmoja Sh. 100,000/- kwa mwezi na kuruhusu mifugo kuchungwa hifadhini kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo kila mfugaji hutozwa kati ya Shilingi milioni sita hadi saba.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Kilyamatundu, Shija Imeli (kulia) alipokuwa akiwasilisha malalamiko yake kuhusu tuhumu za kuwapa rushwa ya shilingi milioni 5.8 Askari watano wa Wanyamapori wa Pori la Akiaba Uwanda (pichani) ili alishe mifugo yake kwa kipindi cha miezi mitano ndani ya pori hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa, wakikagua mazingira ya Pori la Akiba Uwanda baada kuwasimamisha kazi maafisa na askari wote 27 wa pori hilo kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili. Watumishi hao wananalalamikiwa kupewa rushwa ili kuruhusu wananchi wachunge mifug hifadhini na kwa wale ambao hawatoi rushwa huishia kukamtwa mifugo yao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa, wakikagua mazingira ya Pori la Akiba Uwanda baada kuwasimamisha kazi maafisa na askari wote 27 wa pori hilo kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili. Watumishi hao wananalalamikiwa kupewa rushwa ili kuruhusu wananchi wachunge mifug hifadhini na kwa wale ambao hawatoi rushwa huishia kukamtwa mifugo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...