Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Waziri wa maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amesema hatamfumbia macho mfanyakazi atakayezembea kazini kwa namna yoyote badala yake atamsafisha mara moja na kumtoa kabisa kwenye idara na kumuhamishia hata chuoni.
  
Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo wakati alipotembelea ofisi za Dawasa zilizopo Mwanayamala jijini Dar es Salaam.

“Tunataka kufanya maendeleo, sitamtoa mtu kwa kumuonea nikikuona wewe umekaa pale na miradi yetu uliyochelewesha nitakuacha,  kwa nini nikuache, najua utafanya vile vile, na sitakuacha kwenye idara, nitakupeleka chuo cha maji, si kwa ajili ya kuwakomesha wanafunzi hapana, ila sitamuacha mtu aliyefanya ujinga aendelee”.

Amesema, uteuzi huu ni heshma kubwa kwani sasa anakwenda moja kwa moja kutatua matatizo ya watanzania ambao hasa ukienda vijijini ndio utajua kuwa kuna watanzania wana shida ya maji.

Amewaasa wafanyakazi hao kuwa na lengo la pamoja la kuhakikisha wanamsaidia Mtanzania yule masikini, kuweza kupata maji 
“Tunasema tumtue mama ndoo kichwani kwa kumpelekea maji karibu”.

“Ninaamini tukiungana wote kwa pamoja tutaweza, hakuna jambo lisilowezekana, muhimu ni kujipanga na kuwa na nia thabiti ya kuwasaidia watanzania kupata maji.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), wakati akiwasili kuzungumza nao makao makuu ya mamlaka hiyo, Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) leo alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakimsikiliza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa alipotembelea ofisini hapo leo.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa(kushoto) akizungumza na  Mkurugenzi wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja alipotembelea katika ofisi za  DAWASA leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiagana na wafanyakazi wa DAWASA  mara baada ya kumaliza ziara yake katika ofisi za mamlaka hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...