Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND) umeridhishwa kwa kiasi kikubwa na Jinsi Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika kupambana na magonjwa hayo.
Pamoja na hayo Wawakilishi wa Mfuko huo hapa Nchini wamesema kuwa kutokana na mwenendo mzuri wa Tanzania katika kutumia viozuri Mfuko huo sasa wanaweza kuanzisha kitu kingine kizuri kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya na kupeleka mapendekezo na kukubaliwa.
Malengo ya kikao hiko kikao kati ya Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND) na Wizara ya Afya ni kujadili ,kupanga na kuboresha Sekta ya Afya nchini.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi(GLOBAL FUND)  hawapo pichani kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND)  hapa nchini Dkt. Sai Kumar kulia akimueleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha kujadili mambo mbalimbali ya afya kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia  akizungumza na Naibu Waziri wake Dkt. Faustine Ndugulile kushoto wakati wa kikao na wawakilishi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND)  hawapo pichani kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND) kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.
PICHA NA WIZARA YA AFYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Ummy,
    Hawa global Fund walitoa udhamini kwa wanafunzi wa masomo ya ukunga.Moja ya mashart waliyotoa kwenye mkataba ambao walezi walisaini ni kwamba wakishamaliza Masomo yao watapelekwa moja kwa moja kwenye vituo vya kazi kwa mkataba.Kila mwanafunzi alielekezwa kuwa ataenda kufanya kazi wilaya fulani.
    Toka wahitimu,hawajapata maelekezo ya namna gani watakwenda huko.Kiufupi hakuna kilichofanyika na wazazi na walezi wa vijana hawa hawajataarifiwa lolote.Je hili limekaaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...