Na Woinde Shizza, Arusha

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Karatu  kimeonya baadhi ya watendaji wanaohujumu miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji ,barabara ambayo inalenga kutatua changamoto za wananchi. 

Mwenyekiti wa CCM wilayani hapo Lucian  Akonaay ametoa onyo hilo jana ambapo amesema  wanaohujumu miradi watachukuliwa hatua.

Amesema kuwa wananchi bado wana imani na chama hicho katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma muhimu za kijamii ikiwemo maji na miundombinu ya barabara pamoja na huduma za afya.

Akonaay amesema kuwa Chama hicho kimeandaa utaratibu wa kutembelea miradi ya maendeleo  na kujihakikishia kuwa iwapo inatekelezwa kwa viwango stahiki na kwa wakati uliopangwa

 Kwa upande wake Katibu wa CCM Karatu  Solomon Itunda amesema kuwa viongozi wa chama hicho wamekua wakikagua maendeleo ya miradi pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora ikiwa ni pamoja na kutoa mapendekezo kwa viongozi wa Serikali.

Diwani Mteule wa Kata ya Baray kupitia  Chama hicho Elitumaini Rweyemamu amesema kuwa wamejiandaa kusimamia utekelezaji na kutatu kero za wananchi ili kuboresha huduma za kijamii.
 Wakati huo huo Mkazi wa Karatu ameipongeza Serikali kwa kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa kuchimba visima na kuiomba iongeze visima na mabomba hususan kwenye maeneo yenye watu wengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...