Naibu Waziri  wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Abdalla Ulega akiongozana na Dkt. Rashid Tamatama Katibu Mkuu Uvuvi wamezungumza na watumishi wa upande wa Mradi wa SWIOFish katika ukumbi wa Mvuvi House - Dar es Salaam.

 Mh. Naibu Waziri baada ya kupata maelezo kuhusu Mradi huo  ametoa changamoto kwa watendaji kwa kuwaeleza kuwa elimu inayotolewa kwa jamii za wavuvi iweze kuleta matokeo chanya hata pale mradi utakapo maliza muda wake na kuwepo na matokeo ambayo yataweza kupimika hata kwa macho. 
Hii itasaidia sana jamii zetu ambazo Mara nyingi miradi ikiishà na wao hali zao zinaendelea kuwa duni badala ya kuwa zimeboreshwa.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo leo jijini Dar as Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...