DC Mfaume awaahidi makubwa, awapongeza
CHAMA cha Walimu Tanzania(CWT) wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wamekumbushwa kwamba chama hicho ni kwa ajili ya kutetea maslahi ya walimu.
Wameambiwa hicho si chama cha kiuanaharakati wala chama cha siasa na kwamba wajikite kwenye lengo lao la msingi. Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume amewaambia viongozi wa chama hicho leo kuwa Serikali inatambua changamoto zinazowakabili walimu zikiwemo upandaji wa madaraja na madai mengine.
Amewatoa wasiwasi kwamba madai yao yanashughulikiwa huku akiahidi kuendelea kuboresha mazingira yao ya kazi ikijumuisha na miundombinu Pia Mfaume amewakumbusha CWT kwamba katika moja ya ziara alizofanya, wazazi walilalamika kuhusu adhabu kali zinazotolewa kwa wanafunzi shuleni. " Mfano adhabu ya kuwafyatulisha wanafunzi matofali 1000 wanapofanya makosa.
Hivyo nituwaombe walimu kutumia busara adhabu wanazotoa mashuleni... "Kwani wasipotumia busara tatizo la utoro kwa wanafunzi litaongezeka," amesema Mfaume huku akiwapongeza kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya. Ameongeza na hasa ikizingatiwa kwamba ufaulu wa wanafunzi hasa wa sekondari ni wa kuridhisha.
Mfaume amewaahidi CWT ushirikiano wa kutosha na kuwasihi waendelee kuchapa kazi. Mkuu wa Wilaya huyo amekuwa akitumia muda msingi akifanya ziara ya kutembelea na kukagua maeneo mbalimbali. Ambapo lengo lake kubwa ni kuhakikisha anasikiliza kero za wananchi wa Namtumbo na kisha kuzipatia ufumbuzi kwa kushirikiana na viongozi wengine wa Wilaya hiyo.

Mkuu
wa Wilaya ya Namtumbo,Mh Sophia Mfaume (tatu kulia) akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha Walimu Tanzania (CWT)
wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma,mara baada ya kuzungumza nao
Baadhi
ya Waalimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh Sophia Mfaume
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wilayani humo kuhusu mambo
mbalimbali ikiwemo na kuelezwa kuwa cha hicho si kiuanaharakati
wala si chama cha siasa na kwamba wajikite kwenye lengo lao la msingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...