Benny Mwaipaja, WFM, Kigoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kigoma kufanya uchunguzi na kuchukua hatua baada ya kubaini harufu ya ufisadi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 9 ya shule ya msingi Kigoma yanayojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya shilingi milioni 200.

Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo baada ya Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Dkt. John Tlatlaa, kueleza kwamba mradi huo unahusisha ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa na vyoo vyenye matundu 12, wakati mkataba ulioingiwa kati ya Manispaa na Mkandarasi inayoonesha kwamba yatajengwa madarasa tisa na vyoo vyenye matundu 12.

Baada ya mjadala kati yake na Kaimu Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Kigoma, akamwelekeza Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Mwanamvua Mlindoko kuchukua hatua za kiuchunguzi.

"Mradi unaojulikana Mhe. Mkuu wa Wilaya ni wa madarasa tisa, mkandarasi akija kudai nyongeza ya malipo kwa darasa moja lililoongezeka atakuwa na haki!, ninachokichukua mimi ni taarifa hii inayoeleza kujengwa kwa madarasa tisa, hilo moja ni la kwake Mkurugenzi kichwani" alisisitiza Dkt. Kijaji

Aidha, Dkt. Kijaji alibainisha kutoridhika kwake na gharama za ujenzi wa darasa moja kwa shilingi 17m na kwamba kiasi cha shilingi milioni 200 kilichotolewa na Japan kutekeleza mradi huo kingeweza kujenga madarasa hata 20.
Sehemu ya msingi wa vyumba vya madarasa mapya yanayojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, katika Shule ya Msingi Kigoma, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkoani Kigoma, kwa gharama ya zaidi ya shilingi 200m
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (Mbele), akiwa na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, pamoja na wataalam wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, alipofanya ziara kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 9 yanayo jengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 200 katika Shule ya Msingi Kigoma, iliyoko Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (Katikati), akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 200 katika Shule ya Msingi Kigoma, iliyoko Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Dkt. John Shauri Tlatlaa, akitoa ufafanuzi wa idadi ya vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Kigoma kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), ambao unatofautiana na maelezo ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Sabasi Lugai, aliyetoa taarifa kwamba yako tisa, jambo lililosababisha Naibu Waziri huyo kuagiza kufanyika kwa uchunguzi wa mradi huo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...