Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango amewaaga watumishi watano wa wizara hiyo wanaosafiri kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya ufadhili wa Masomo, uliotolewa na DFID Kupitia mfuko wake wa UKAID.
Akizungumza na Michuzi Media Group katika Mkutano wa kuwaaga watumishi hao, Waziri Mpango aliwataka Vijana hao kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutokubali kuyumbishwa na jambo lolote la ujanja kutoka kwa watu wa Mataifa mengine.
“Hii nafasi niliomba mimi kwa ajili ya watumishi wa Wizara muende kujifunza na hili ni kundi la pili ,hivyo naomba mkafanye kile kilichowapeleka kwani watanzania zaidi ya Milioni Hamsinii wanategemea kuja kunufaika na ujuzi mlioupata kutoka huku ili muweze kuja kuendesha taasisi hii,ambayo ndio Ubongo wa uchumi wa nchi yetu” alisema Dkt. Mpango.
Dkt MPango alisisitiza kuwa yeye kama Waziri anajivunia sana kuona Vijana wanapanua maarifa kwa kujiongezea elimu kutoka sehemu nyingine ,kwani kunasaidia kujiamini na kuzungumza kwa hoja za uhakika mbele ya umati wa watu.Alisema kuwa kama watalaamu wote hao kutoka wizara ya fedha watafanikiwa kufanya vizuri, watazidi kuiongezea sifa nchi yetu kuendelea kupata nafasi ya kupeleka vijana wengi kwenda kujifunza.
Ameweka wazi kuwa yeye atakuwa Waziri mwenye furaha sana kwa kuona kila idara katika Wizara yake ina vijana makini ambao ni weledi katika kazi zao.
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akizungumza na Vijana watano kutoka Wizara hiyo ambao wamepata ufadhili wa masomo nchini Uingereza
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akisisitiza jambo kwa Vijana hao
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akiagana na Vijana hao na kuwatakia Safari Njema
Wafanyakazi wa Wizara ya fedha , Sudah Joseph, Peter Kalugwisha,Morick Mwasagwa,Eliud Mkilamweni na Tunsume Mlawa wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya Pamoja na Wanufaika wa Ufadhili wa Masomo wa DFID kupitia Mfuko wa UKAID
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...