WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemaujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Tazara umekamilika kwa asilimia 98 na itafunguliwa Oktoba mwaka huu na Rais Dkt. John Magufuli.


Mradi wa barabara ya juu (Mfugale flyover) chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani, unalengo la kupunguza msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere.Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29 ,2018) baada ya kukagua ujenzi wa mradi huowa barabara ya juu katika eneo la Tazara jijini Dar Es Salaam. 

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa kazi ya umaliziaji wa mradi huo inayoendelea kwenye hilo.“Mradi utapunguza muda wa usafiri katika barabara ya Nyerere hususani kwa wananchi wanaotoka katikati ya jiji kwenda uwanja wa ndege na wanaotoka Buguruni, Temeke.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi Mkoa wa Dar Es Salaam watafute eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo ili waweze kuondoka kandokando ya barabara hizo za juu zinazojengwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe kuhusu barabara ya juu ya TAZARA wakati alipokagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara ya juu ya eneo la TAZARA wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale kuhusu ujenzi wa barabara ya juu ya eneo la TAZARA wakati alipokagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaaam, Paul Makonda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la TAZARA jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wa barabara za juu katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...