Wataalam wa afya kutoka nchini Japan leo wametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali hiyo.
Katika mazungumzo yao watalaam hao wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu wa utoaji huduma za afya na kujadiliana namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma .
Mkurugenzi wa huduma za tiba Dkt. Hedwiga Swai amesema MNH ina mipango mbalimbali ya kuboresha huduma zake za ubingwa wa juu ikiwemo upandikizaji figo na kusisitiza kuwa huduma hiyo ni endelevu na imekuwa na mafanikio makubwa tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini Novemba mwaka jana .
“Lengo letu ni kuhakikisha huduma za kibingwa zinakuwa endelevu lakini pia kama hospitali mipango yetu ni kuanzisha huduma zingine mpya ambazo hapo awali hazikuwepo”amesema Dkt. Swai.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za tiba shirikishi Dkt. Praxeda Ogweyo amesema pamoja na mafanikio ambayo Muhimbili imepata lakini pia kuna changamoto ya upungufu wa watalaam katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma
Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na wataalam wa afya kutoka Japan wakijadiliana juu ya utoaji wa huduma bora za afya .
Mmoja wa wataalam kutoka Japan Yoshio Mikamo akielezea ambavyo huduma za afya zinatolewa nchini humo.
Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya Hospitali ya Taifa Muhimbili wakisikiliza maelezo yanayotolewa na mtaalam huyo.
Mkuu wa Idara ya Famasia MNH Deus Buma akiwaelezea wataalam hao kuhusiana na huduma za utoaji dawa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mara baada ya kutembelea moja ya maduka ya dawa ya hospitali hiyo.
Meneja wa jengo la wagonjwa wa nje Sista June Samwel akifafanua
huduma zinazotolewa katika jengo hilo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...