Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
MBUNGE wa Jimbo la Manonga, Mheshimiwa Seif Gulamali amewataka viongozi na watendaji wa serikali kutokujihusisha na ubadhilifu wa fedha za miradi ambayo imepangwa kwa maendeleo ya wananchi.

Akihutubia wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo wakati wa ziara yake kwa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoani Tabora amesisitiza na kueleza kuwa akiwa mwakilishi wa wananchi hatakubali kuona wizi, ubadhilifu au ufujali wa fedha za maendeleo.

Mh. Gulamali ameeleza kwamba vitendo vya mazoea vilivyokuwa vikifanywa na watendaji wa serikali wakishirikiana na wakandarasi katika kupitisha miradi ya maendeleo isiyo na ubora na iliyo chini ya kiwango vimepitwa na wakati. Amesema kuwa, Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Rais John Joseph Magufuli imejikita katika uwazi na kuhudumia wananchi wanyonge dhidi ya dhuluma.

Katika ziara hiyo ya ALAT Mkoa wa Tabora, Gulamali alipongeza matumizi mazuri ya fedha za ujenzi na ukarabati wa kituo cha Afya Upuge ambapo takribani milioni 500 katika utekelezaji wa maradi huo, mradi huo umehusisha ujenzi wa maabara mpya, chumba cha kuhifadhia maiti, Nyumba ya Mganga, Jengo la Mama na Mtoto pamoja na njia za ndani ya Kituo cha Afya.

Aidha Mbunge huyo amechangia kiasi cha shilingi laki tatu katika ujenzi wa shule msingi katika kijiji cha Mbola Wilayani Uyui mradi ambao unatekelezwa kwa michango ya wananchi huku ukilenga kupunguza adha kwa wanafunzi toka kitongoji cha Migazini kutembea umbali wa Kilometa 14 kuifuata shule.

Pia wajumbe wa ALAT mkoa wameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kuunga mkono juhudi za wanakijiji wa Mbola katika ujenzi wa shule.

Katika kuhitimisha ziara yake, Mheshimiwa Gulamali alitembelea Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mihayo(St. Mary Mihayo Tabora) waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete baada ya kujeruhiwa na moto uliounguza sehemu ya shule hiyo usiku wa tarehe 28, Gulamali ambaye alipata kuwa mwanafunzi katika shule hiyo ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika kupitia miundo mbinu hasa ya umeme katika shule hiyo.

Wakiongea na mwandishi wetu Wazazi na Wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo wameeleza kufarijika sana na jinsi Mbunge huyo alivyoonesha kuwajali na kuwatembelea mara baada ya kupatwa na janga hilo.
Mbunge wa Manonga Mh. Seif Gulamali akisalimiana na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Uyui bw. Makoba Lubasha mara baada ya mkutano na viongozi wa ALAT kumalizika.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akitoa pole kwa wazazi wa watoto wa shule ya Sekondari Mihayo ambao walipata janga la moto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...