Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea kote nchini pamoja na kuweka udhibiti imara wa upotevu wa fedha ili kusiwe na upungufu wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma nchini. 

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na wa Halmashauri zote nchini uliofanyika katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.“Fanyeni kazi kwa weledi kwani msipotimiza wajibu wenu ipasavyo tudumaza afya za wananchi, natamani itakapofika mwaka 2020 kila mwananchi azungumze faraja kwenye sekta ya afya”, alisema Waziri Jafo.

Aidha,Waziri huyo alisema katika ukusanyaji wa mapato hauridhishi, hivyo kufanya vituo vingi kuwa na makusanyo madogo ya mapato ya kila siku licha ya kuwahudumia wananchi wengi. Kwa upande wa kuboresha huduma za afya nchini, Waziri Jafo alisema wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani kulikuwa na vituo vya afya 115 vilivyokuwa na uwezo wa kufanya upasuaji wa dharura.

Kwa sasa vipo vituo 210 ambavyo vinatoa huduma hiyo , sawa na asilimia 95 Aliendelea kufafanua kuwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 Serikali imetenga takribani bilioni 105 ambapo ajenda kubwa ni ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 hivyo kufanya vituo 307 vitakavyokuwa vinafanya upasuaji wa dharuara. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akisistiza Jambo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dk. Zainabu Chaula akitoa mada katika Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akihimiza umuhimu wa matumizi ya takwimu afya kwenye Mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma wakimsikiliza Mgeni rasmi ( hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...