Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amewataka watu wenye viwanda kulipa tozo za shilingi 10 kwa lita ambapo baadhi yao wameshindwa kutekeleza agizo hilo licha ya kuwepo kwa sharia hiyo.

Kushindwa kulipa huko kunatokana na kiwango hicho kuwa kikubwa na kufanya sheria hiyo ishindwe kutekelezwa .

Hayo aliyasema jijini Dar es Salaama katika mkutano wa wadau mbalimbali ulioandaliwa na Bodi ya Maji ya Bonde la Mto Wami/ Ruvu kujadili tozo hiyo ambapo alitaka kufikiwa mwafaka kwa ajili ya kuanza kulipa kama sheria inavyotaka au kupunguza tozo.Amesema Wizara ilifanya mabadiliko ya viwango vya ada za matumizi mbalimbali ya maji vilivyokuwa vinatumika kuanzia mwaka 2002.

Profesa Mbarawa amesema kuwa kiwango cha tozo cha shilingi 10 kwa lita ya kilitangazwa katika gazeti la serikali na kwamba taarifa ya kawaida namba 783 ya Agosti, 2013 kilianza kutumika mwaka wa fedha 2014/2015.

"Hatua hii imefikiwa baada ya ada za awali kuwa ndogo ikilinganishwa na gharama halisi za usimamizi wa rasilimali maji.Tangu kipindi hicho baadhi ya yenu wenye viwanda mmeshindwa kutekeleza agizo hili na kuwa na sheria isiyotekelezwa hakuna maana kuendelea au ifutwe,"Waziri Mbarawa.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akifungua mkutano wa kujadili tozo za matumizi ya maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji wa Wizara hiyo George Lugomela akizungumza katika mkutano wa kujadili tozo za maji pamoja na maendeleo ya bodi katika usimamizi vyanzo vya maji uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani akizungumza kuhusiana usimamizi wa vyanzo vya maji katika mkutano wa kujadili tozo za maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masasi Food Industry wazalishaji wa Maji ya Lulu Charle’s Zakaria akizungumza kuhusiana na tozo hiyo biashara hiyo kuwa ni kubwa hivyo kikao kitafikia mwafaka katika mkutano wa kujadili tozo za maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika mkutano wa kujadili tozo za maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...