KAMPUNI ya Sukari ya Kilombero (KSC) imezindua paketi ndogo za sukari yake ijulikanayo kama ‘Bwana Sukari’, ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanamudu kununua sukari hiyo kutokana na unafuu wake wa bei.
Paketi mpya za sukari chapa ya ‘Bwana Sukari’ zinapatikana kwa ujazo wa gramu 350 maarufu kama ‘Robo Plus’ na paketi za gramu 160 maarufu kama ‘Booster’.
Paketi za ‘Robo Plus’ zitauzwa shilingi 1,000/ kwa kila paketi, na paketi za ‘Booster’ zitauzwa kwa shilingi 500/-kwa kila paketi.
Uzinduzi wa paketi mpya za ‘Bwana Sukari’ uliofanyika maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya KSC kuhakikisha sukari yake inawafikia watanzania wa hali mbalimbali za kiuchumi.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Chama cha Wazalishaji wa Sukari Tanzania (TSPA), viongozi na wafanyakazi wa KSC.
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akizungumza na wananchi wa Mbagala siku ya uzinduzi wa paketi ndogo za sukari ya 'Bwana Sukari' inayozalishwa na kiwanda hicho. Paketi hizo zitauzwa kwa shillingi 500/- na shillingi 1000/-.
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akimkabidhi paketi mpya za Bwana Sukari mkazi wa Mbagala Zena Athumani siku ya uzinduzi wa bidhaa hiyo uliofanyika viwanja vya Mabagala Zakeem hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari siku ya uzinduzi wa paketi ndogo za sukari ya Bwana Sukari itakayouzwa kwa shillings 500/- and shillingi 1000/-.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...