Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Agosti 13, 2018 kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili  aliyekuwa mhasibu wa Takukuru, Godfrey Gugai anayekabiliwa na  tuhuma ya utakatishaji na kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomka bili yeye na wenzake watatu.

Kesi hiyo leo Agosti 6, 2018  ilikuja kwa ajili ya shahidi Ayoub Akida wa upande wa mashtaka kuendelea kutoa ushahidi wake ambao alisimama kuutoa kutokana na kubishania kielelezo cha barua ya kufutwa kazini kwa Gugai.

Hata hivyo, wakili wa serikali kutoka Takukuru, Vitalis Peter ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shahidi huyo amepata udhuru.

Aidha imedaiwa wakili wa utetezi Alex Mgongolwa amefiwa na mdogo wake, Na hivyo mahakama kulazimika kuiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.

Inadaiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh 3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa cha zaidi ya  Tsh.milioni 800,huku akishindwa kuzitolea maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...