Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuuliza maswali Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara mjini, Ibrahim Mhando (kushoto) baada ya kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye ni mshauri mkuu wa ujenzi wa Ofisi Kuu ya Uhamiaji Mkoani Mtwara. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoka Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara mara baada ya kumsweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi hicho ambaye aliwaweka watuhumiwa chumba cha upelelezi badala ya mahabusu kituoni hapo. Nyuma ya Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuangalia Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Lucas, ambaye pia kandarasi aliyejenga Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Theophilius Kessy, wakati alipokua anambana maswali ya kutaka kujua kwanini Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara limejengwa chini ya kiwango. Aliyeshika kitabu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
                                                                                                                         
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye alitoa taarifa ya uongo kwa Waziri huyo kuhusu ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji Mkoani humo.

Tukio hilo lilitokea saa 12:46 asubuhi Agosti 27 leo Jumatatu, wakati Waziri Lugola na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali, Jacob Kingu walipofika Kituo hicho kikuu cha mkoa kwa kushtukiza wakati alipokua anakwenda Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es Salaam, ndipo Waziri huyo alitaka kuthibitisha kama mtuhumiwa ambaye alielekeza jana usiku akamatwe awekwe mahabusu endapo Polisi walitekeleza agizo lake.

Hata hivyo, Waziri Lugola alimkuta mtuhumiwa huyo, Benjamin Kasiga akiwa chumba cha upelelezi badala ya kuwekwa mahabusu ya polisi hiyo, ndipo akamuuliza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Lucas Mkondya, kwanini agizo lake halijatekelezwa.

“Hivi ndivyo polisi mnafanya hivi, haya ndio madudu mnayoyafanya? Tabia hii siku zote tunaipinga ikichafua Jeshi la Polisi, na hii ndiyo tabia yenu, najua ndio mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi? RPC hawa polisi wako wanafanya nini, OCS njoo hapa, kwanini umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi huyu,” alisema Lugola akiwa amekasirika. 

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo (RPC), Mkondya alimweleza Waziri Lugola kituoni hapo kuwa, Polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.

Kwa upande wake mkuu wa kituo huyo, Mhando kabla ya kuwekwa mahabusu pamoja na wale watuhumiwa ambao alishindwa kuwaweka mahabusu, alisema sababu kuu yakutowaweka mahabusu watuhumiwa hao ni kwasababu mahabusu ilijaa na wanafanya hivyo mara chache inapotokea mahabusu wamekuwa wengi kituoni hapo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...