WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo Ijumaa, Oktoba 31, 2018 kuelekea nchini China kumuwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika  na China  (FOCAC)

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini Beijing nchini China, ambapo utafunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping. Katika mkutano huo Waziri Mkuu anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli. 

Mbali na kuhudhuria mkutano huo pia, Waziri Mkuu anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa kampuni mbalimbali akiwemo Rais wa Kampuni ya CCECC, Rais wa Shirika la NORINCO, Rais wa Kampuni ya Zijin Gold Mine pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya saruji ya HEGNYA.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akienda China kumuwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika  na China  (FOCAC), Agosti 31, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akienda China kumuwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika  na China  (FOCAC), Agosti 31, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka nichini kwenda China kumuwakilisha Rais John Magufuli  Katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC), Agosti 31, 2018. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...