Na Jumia Tanzania
Katika ya dini ya Kiislamu, Eid Al-Adha au ‘Sikukuu ya kuchinja’ ni sikukuu kubwa inayofanyika baada ya kuisha kwa Hija. Sikukuu hii huashiria kuisha kwa ibada ya Hija eneo la Mina, nchini Saudi Arabia, lakini huadhimishwa na Waislamu duniani kote kama ishara ya kumbukumbu ya imani aliyoionyesha Ibrahimu.
Eid Al-Adha huanza siku ya kumi ya Dhu’l-Hijja, mwezi wa mwisho kwenye kalenda ya Kiislamu, na hudumu kwa muda wa siku nne. Huanza baada ya siku ambayo Waislamu kumali Hija wakishuka kutoka Mlima Arafat.

Sikukuu hii husherehekewa na Waislamu duniani kote, kama zilivyo tamaduni za imani ya dini nyingine. Lakini Eid Al-Adha ni nini? Yafuatayo ni mambo matano ambayo Jumia ingependa uyafahamu kuhusiana na sikukuu hii.
Historia ya Eid. Eid Al-Adha, ni sikukuu ya Kiislamu inayoadhimishwa kukumbuka tukio la Nabii Ibrahimu kuwa tayari kumtoa sadaka mwanaye wa pekee kwa kuchinja kama alivyoagizwa na Mungu. Ingawa alikuwa ni mtu mwema na aliyempenda mwanawe; imani yake na kujitoa kwa Mungu vilikuwa na nguvu zaidi kiasi ambacho angeweza kufanya chochote alichoagizwa. Kitendo cha utayari wa Ibrahimu kumtoa sadaka mwanaye wa pekee kwa Mungu kilipelekea Mungu kutoruhusu kuchinjwa kwa mtoto yule na badala yake akampatia mwanakondoo kuwa mbadala.

Kitendo cha kuchinja mnyama. Kwa wengi walio nje ya imani ya Kiislamu wamekuwa wakilitafsiri hili tukio tofauti. Kinyume chake, Waislamu huwachinja wanyama wao kwa kutanguliza sala kwanza na kuwachinja kwa jina la Mungu, ambaye amewapa mamlaka juu ya wanyama hao na haki ya kuwala. Hata hivyo, Wailsamu wanapolitaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja, ni kutukumbusha kwamba uhai ni kitu kitakatifu. Kwa hiyo kiuhalisia, hukifanya kitendo hiko kwa kumbariki mnyama na kumshukuru Mungu, pamoja na kutambua utakatifu wa maisha ya mnyama.

Nyama hugawiwa kwa familia, jamaa na maskini. Eid Al-Adha pia hujulikana kama ‘Sikukuu ya Kuchinja.’ Kondoo, ng’ombe, mbuzi, au ngamia ni sadaka kwa jina la Mwenyezi Mungu. Nyama itokanayo na sadaka hugawanywa katika mafungu matatu: theluthi moja kwa ajili ya familia, theluthi nyingine kwa marafiki na majirani, na theluthi inayobakia hugawiwa kwa maskini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. I Visit Your Blog This Is so Impresive. And I read Your All Article. Your Work Is Very Good Your Article Writting Is Professional I realy Like Your Work and Situs Judi Slot Gacor SLOT1288 bandar judi online terbaik Indonesia tahun 2021 yaitu SLOT1288. Situs Slot GACOR selalu memberikan promo welcome bonus 100% untuk member baru dan Promo Deposit Pulsa Tanpa Potongan Bonus 10%

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...