Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MICHUANO ya Ndondo Cup yamefikia tamati leo baada Timu ya Manzese United kuibuka mabingwa wapya wa Ndondo Cup 2018 baada ya kuifunga timu ya Kivule kwa goli 1-0 mechi iliyofanyika leo Jijino Dar es Salaam.

Mchezo huo ulioanza majira ya 10 alasiri katika uwanja wa Bandari ulichezeshwa na Mwamuzi mwenye beji ya FIFA Hery Sasii akisaidiwa na Mwamuzi wa pembeni Soud Lila na Hellen Mduma.Mchezo huo ulianza kwa kasi katika dakika ya 9 Manzese United wanapata goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Hamza lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

Umakini wa safu ya ushambuliaji ya Kiluvya United iliwanyima fursa ya kusawazisha goli hilo ambapo waliweza kukosa nafasi nyingi za wazi.Kipindi cha pili kilianza Kiluvya wakisaka goli la kusawazisha ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika Manzese walifanikiwa kushinda goli 1-0 na kuwa mabingwa wapya wa Ndondo Cup.

Mgeni rasmi wa mashindano Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shoza aliweza kukabidhi kombe kwa mabingwa wapya wa Ndondo Cup akiwa ameambataba na viongozi mbalimbali Nchini.

Fainali hiyo ya kipekee ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mbunge wa Iramba Mashariki Mwingulu Nchemba aliyekabidhi hundi ya Milioni 10 kwa mabingwa, Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, Mkuu wa Wilaya Temeke Felox Lyaniva, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu, Rais wa TFF Wallace Karia na Mwenyekiti wa DRFA Almas Kasongo.

Mbali na hao pia Manzese waliwakilishwa na Meya wa Jimbo la Ubungo Boniface Jacob na wasanii wanaoishi kwenyr jimbo hilo Akiwemo Msanii Madee na Shilole sambamba na viongozi wengine wa kimpira.

 Mbunge wa Iramba Mashariki Mwigulu Nchemba akikabidhi  mfano wa hundi yenye thamani ya Milioni 10 kwa Nahodha wa timu ya Manzese baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Kivule United

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akikabidhi kombe kwa Nahodha wa Manzese United baada ya kuibuka na ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Kivule United katika Mchezo uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 

Mchezaji wa Manzese United Idd Nado akiwa amemlaza chini mchezaji wa Kivule United katika fainali ya Ndondo Cup iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam na Manzese United kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0.
 Kikosi cha Kiluvya United wakiwa katika picha ya Pamoja
Kikosi cha Manzese United wakiwa katika picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...