Na Woinde Shizza,Arusha .
Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amewaahidi watumishi wa halmashauri ya Meru kuwapa ushirikiano wa kuweza
kutimiza majukumu yao ikiwa ni njia mojawapo ya kutoa huduma bora kwa
wananchi .
Hayo aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi, watumishi wa halmashauri hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa halmashauri hiyo ambapo aliwahaidi kuwapa ushirikiano
watumishi wote katika swala zima la kusikiliza na kutatua kero za
wananchi.
"Napenda kuwatoa hofu watumishi wote kwa ujio wangu kwani nitawapa
ushirikiano na kuwawezesha kutimiza majukumu yenu ikiwa ni pamoja na
utoaji wa huduma bora ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano
ya kusikiliza na kuzitatua kero za wananchi pamoja na rasilimali za
Tanzania ili kuwanufaisha wananchi wote hasa wanyonge na watoto wa
maskini, nukuu nimekuja hapa kutimiza torati na si kuivunja" alisema Mhe. Muro.
Alisisitiza kuwa ushirikiano huo utaanza kwa kuwapa fursa watumishi
hao kwa kueleza changamoto zao na kupokea mawazo,maoni na mikakati
itakayoleta maendeleo kwenye halmashauri hiyo na Wilaya ya Arumeru. Alibainisha kuwa anatarajia kufanya kikao kingine Jumatatu Agosti 6 2018.
Awali aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ambaye ni mkuu wa
wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta akimkabidhi ofisi hiyo alisema kuwa
watumishi wa Meru ni wazuri na wachapakazi na amemkabidhi pamoja na
ofisi wakiwa weupe na wenye afya tele pia wanyeyekevu.Mhe. Kimanta aliwawataka watumishi hao kumpa ushirikiano mkubwa mkuu huo mpya
wa wilaya kama walivyompa yeye ili kuweza kuwaletea maendeleo
wananchi wa meru na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Arumeru akiongea kabla ya kukabidhi ofisi kwa DC mpya Mhe. Jerry Muro.
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru wakiwa kwenye kikao hico
Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akiongea kwenye kikao hicho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...