Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Liberates Sabas amesema Jeshi la Polisi kwa sasa linaendesha Operesheni mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Nchi ya Msumbiji ili kuwakabili wahalifu wanaokimbili nchini humu. 

Aidha Jeshi la Polisi kupitia Operesheni Maalum inayoendelea mkoani Mtwara limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 96 kati yao 10 wamefikishwa mahakamani kwa kesi mbalimbali na wengine 16 wamefikishwa katika idara ya Uhamiaji kwa makosa yanayohusu maswala ya uhamiaji katika operesheni hiyo kumepatikana siraha mbili zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu katika maeneo mbalimbali. 

Aidha Afande Sabas amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa kuendelea kutoa ushirikiano mzuri ndani ya Jeshi la Polisi na kuwataka wananchi wote nchini kuendelea kutoa ushirikiano ili kutokomeza uhalifu nchini. 
Mkuu Wa Operesheni Maalum za Jeshi La Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberates Sabas, akikagua na kuangalia silaha zilizokamatwa na askari Polisi katika operesheni maalum ya kutokomeza uhalifu nchini inayoendelea mkoani Mtwara. (Picha na Jeshi la Polisi) 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...