Na John Mapepele

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua mikakati 15 itakayotumika kama nyenzo ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo na kuleta mageuzi makubwa na ya muda mfupi kwenye sekta za mifugo na uvuvi kabla ya kumalizika awamu ya kwanza ya utawala wa Serikali ya awamu ya tano mwaka 2020.

Mikakati hiyo ni pamoja nakudhibiti magonjwa ya mifugo chanjo na viatilifu, mpango kazi wa kudhibiti upotevu wa mapato yatokanayo na biashara ya mifugo na mazao yake, mkakati wa usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi nchini, mkakati wa upatikanaji wa uhakika wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo pamoja na mkakati wa kuboresha na kuzalisha kwa wingi ng’ombe wa nyama na maziwa kwa njia ya uhimilishaji.

Mwingine ni mkakati wa kudhibiti na kuondoa migogoro baina ya wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi, mkakati wa kuboresha uzalishaji wa kuku,mkakati wa kuanzisha na kuwezesha ushirika wa wafugaji, mkakati wa kuendeleza ukuzaji wa viumbe kwenye maji pamoja mkakati wa kufufua Shirika la Uvuvi nchini TAFICO

Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mikakati hiyo, Waziri Mpina ameiagiza wizara hiyo kuunda kikosi kazi kitakachosimamia utekelezaji wake na kwamba kila baada ya miezi mitatu kufanyike tathmini na kwa watumishi wataoshindwa au kukwamisha utekelezaji wa mikakati hiyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria,Kanuni na taratibu. 

Alisema mikakati hiyo ikikamilika Serikali itaweza kukusanya zaidi ya sh bilioni 100 kwa mwaka zitokanazo na sekta za mifugo na uvuvi tofauti na sh bilioni 30 zilizokusanywa katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ambapo kwa mwaka 2017/2018 Serikali imeweza kukusanya sh bilioni 46 baada kufanyika Operesheni Sangara na Nzagamba.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwaonyesha Mkakati wa kudhibiti upotevu wa mapato yatokanayo na biashara ya mifugo na mazao yake baada ya kuuzindua katiika ukumbi wa VETA Dodoma. Picha na John Mapepele
Kikosi kazi kilichoandaa mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo nchini kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ( aliyekaa katikati)kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Bi Selina Lyimo, kushoto Kaimu Katibu Mkuu Uvuvi Bwana Julius Mairi.Picha na John Mapepele .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...