Na WAMJW Dodoma

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba ameyataka wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutilia mkazo katika kutekeleza Sera za Maendeleo zilizopo katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) ili kufanikisha juhudi za Serikali katika kuletea wananchi Maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa Mashirika hayo yanapaswa kuwasilisha mipango yao kwa Msajili ili kuweza kuwa na Mpango mkakati mmoja wa kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Ameongeza kuwa suala la Maendeleo ni mtambuka na linapaswa kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Wadau na wananchi ili kufanya shughuli za Maendeleo kuwa endelevu.

 Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Jijini Dodoma katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Idara Kuu Maendeleo ya Jamii pamoja na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa kuhusu ushirikiano kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Serikali katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...