Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, ndugu Alpha Mria akielezea kwa undani namna mchakato huu wa kupata vijana wenye vipaji na mapenzi kwenye sekta ya Filamu na mwisho kupatikana washindi hawa wane ambao mnamo Octoba 2018 wataenda kuiwakilisha Tanzania kwenye ya Mafunzo Maalum ya Tasnia ya Filamu MultiChoice Talent Fatory, huko Jijini Nairobi Kenya kwa kipindi cha mwaka mzima.
Meneja Uendeshaji MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo pamoja na Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria wakiwapongeza vijana hawa wakitanzania walioibuka washindi wa mpango huu wa kukuza tasnia ya Filamu Afrika unaotambulika kama Multichoice Talent Factory, vijana hawa wataliwakilisha Taifa kwenye mauzo haya maalum ya mwaka mzima yatakayofanyika Jijini Nairobi Kenya, kwa ukanda wa Afrika Mashariki yakiwa yameandaliwa na kugharamiwa na MultiChoice Afrika.
Picha ya Pamoja ya Uongozi wa Multichoice Tanzania wakiwa na Vijana walioibuka kidededea watakao kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Mafunzo Maalum ya Filamu Multichoice Talet Factory, jijini Nairobi Kenya, kutoka kusho ni Jamal Kishuri kutokea Arusha, Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, katikati ni Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifuatiwa na mshindi Sarah Kimario  kutokea Dar es Salaam, pembeni ni Menejea Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria na mwisho kulia ni mshindi wetu mwingine Wilson  Nkya kutoka Kigoma wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa halfa hiyo.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania imetawatangaza vijana wanne wa ktanzania waliofanikiwa kushinda shindano la Multichoice Talent Factory watakaoungana na wenzao kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kwa ajili ya kupata mafunzo ya filamu kwenye vituo vitatu tofauti.

Washindi hao waliofanikiwa kushinda wataelekea nchini Kenya kwa ajili ya mafunzo hayo yatakayokuwa ya mwaka mmoja yakianzia Oktoba Mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema kuwa mchakato mzima wa kuwapata washindi hao ulichukua muda wa miezi miwili baada ya kuzinduliwa mwezi Mei mwaka huu, na zaidi ya vija a 160 walituma maombi na mchujo ulifanyika tarehe 20 Julai na kuwapata vijana hawa walioshinda.

Shelukindo amesema kuwa, maendeleo ya nchi kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi zilizopo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori huku sekta ya sanaa na ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo kupelekea mchango mdogo kwenye ukuaji wa uchumi.

Amesema kuwa ili kuhakikisha wanasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya wahimili wa uchumi wa nchi , Multichoice imeweza kuanzisha program hizo na wameanza na sekta ya filamu na tayari wameshapatikana vijana hao watakaoanza mafunzo mwezi Oktoba nchini Kenya.

Shelukindo amewataja vijana hao ni Sarah Kimario kutoka Dar es Salaam, Wilson Nkya wa Kigoma, Jamal Kishuli kutoka Arusha na Jane Moshi wa Kilimanjaro na safari yao tayari imeshapangwa wanasubiriwa kusafiri tu.

Mmoja wa washindi waliotangazwa kufuzu program Sarah Kimario amesema kuwa hii ni moja ya nafasi nzuri ya kuweza kujifunza zaidi masuala ya sanaa na amewaomba wazazi kutokuwakataza watoto wao kufanya kile wakipendacho kwani watakuwa wanashindwa kuonyesha vipaji walivyonavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...