Ni bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Mvula-Mandondo Band yenye makao yake nchini Uingereza,inayoongozwa na mwanamuziki mkongwe wa dansi Mtanzania Saidi Jumanne Kanda aliyewahi kutamba na bendi za Super Matimila, na Bima Lee. mkongwe huyo wa muziki anakiongoza kikosi chake cha Mvula-Mandondo Band katika jukwaa kubwa la maonyesho ya kimataifa ya GaiExpo trade fair yanayoambatana intern.Afrika FestivalTübingen 2018 nchini
Ujerumani ambalo mwaka huu "Focus country Tanzania". bendi ya Mvula-Mandondo Band itapanda jukwaani kuanzia siku ya Ijumaa ya 10 Agosti 2018 hadi Jumamosi 11 Agosti 2018 Maonyesho hayo yanawashirikisha na wajasilimali ,wafanyi biashara,wasanii na wanamuziki na kuwakusanya umati watu zaidi ya laki moja katika viwanja vya Fest-latz,mjini Tübingen,kusini mwa ujerumani.bendi ya Mvula-Mando inatarajia kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa nchini ufaransa mwezi Septemba.usikose kujumuika na waadaau wengine katika maonyesho haya makubwa ambapo wasanii na wajasilia mali toka Tanzania wakiwakilisha na kupeperusha bendera ya "Hapa Kazi Tu"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...