NA. LUSUNGU HELELA-DODOMA
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama Urithi Festival, Celebrating Our Heritage litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesema lengo la Tamasha  hilo  ni kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.

Aidha, Amesema kwa kutambua hazina kubwa ya malikale na utamaduni wa makabila zaidi ya 128 yaliyopo nchini, tamasha hilo litaongeza wigo wa mazao ya utalii kwa kukuza utalii wa utamaduni wa malikale hatua ambayo itaongeza ushindani wa Tanzania kama kituo bora cha utalii kwenye masoko mbalimbali duniani.

Ameongeza kuwa Urithi  Festival itasadia kukuza utalii wa ndani kwa kuongeza muda wa watalii wa kimataifa kukaa nchini kwa vile Tamasha hilo lifanyika katika kipindi ambacho watalii wengi wanatembelea Tanzania.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya   Urithi Festival walioshiriki kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika leo jijini Dodoma. Tamasha hilo linalotarajiwa kuzinduliwa Septemba 15, 2018 na  kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama ‘’Urithi Festival, Celebrating Our Heritage’’ litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.

Baadhi ya Wajumbe wakiangalia  nembo ya Urithi Festival inakayotumika kwenye Tamasha hilo.
  (Picha zote  na Lusungu Helela-WMU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...