Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

REDCROSS Tanzania imedhamiria kuleta mapinduzi kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja anawajibika kutoa msaada wa majanga yanayojitokeza ili kusaidia waathirika wa majanga hayo wasipoteze maisha kwa kukosa huduma ya kwanza.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Redcross Julius Kejo wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana kazi zinazofanywa na Redcross Tanzania na namna kuhakikisha jamii inawajibika kusaidia kuwa mstari wa mbele katika majanga mbalimbali yanayotokea na kuachana na tabia ya kukimbilia kuona bila ya msaada wa huduma ya kwanza.

Amesema bado kuna tatizo kubwa kwa jamii kutowajibika pale yanapotokea majanga ikiwamo ya ajali na mengineyo kwa kushindwa kuwasaidia kwa haraka watu wanaopata athari katika majanga hayo badala yake kubaki washudiaji tu na kupiga picha.

“Ajali ikitokea, badala ya watu kutoa msaada wa huduma ya kwanza kuokoa maisha yao, watu wanawazunguka kuwashangaa, na wengine wanatumia muda huo kuchukua picha kutuma kwenye mitandao na kuacha wenzao wakihangaika au baadhi ya wengine wanapoteza maisha wakati huo huo kwa kukosa huduma ya kwanza wakati pengine wangewasaidi kuokoa maisha yao ,” amesema Kejo

Amesema umefika wakati watanzania kubadilika kujitoa katika kupata elimu ya huduma ya kwanza ambayo itatumika katika kuokoa maisha ya watu katika majanaga mabalimbali kwani kusaidia mtu katika majanga ni haki kwa yule yaliyompata.
 Katibu Mkuu wa Recross Tanzania Julius Kejo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na kazi ya Redcross katika utoaji wa huduma wakati wa Majanga yanapotokea, mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa Ubelgiji Red cross Tanzania An Vanderheyden akizungumza uzoefu wa Redcross katika kujitoa katika uchangiaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...