Waziri wa Madini Dotto Biteko juzi kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo

SERIKALI imesema kuwa itafanya mchakato wa kuleta wataalamu wa utafiti wa miamba(GST),maliasili na mazingira kwa pamoja katika kata ya Mbomole tarafa ya Amani ili kuweza kuona uwezekano wa kuwaruhusu wananchi na wachimbaji wadogowadogo kuchimba madini katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Madini Dotto Biteko alipotembelea katika kijiji cha Sakale katika kata hiyo wakati akizungumza na wananchi waliomuelezea kero yao ya kuzuiwa na serikali kutokuchimba madini eneo hilo licha ya kuwatokuwepo na viashiria vya uharibifu wa mazingira na misitu kama serikali inavyosema.

Wakizungumza kijijini hapo wananchi hao walimueleza naibu waziri huyo kuwa madini katika eneo hilo yaligunduliwa mwaka 2013 na ni mengi yanapatikana kwenye miamba na siyo kwenye chanzo cha mto kama serikali inavyosema lakini walizuiwa kwa tahadhari ya uharibifu wa mazingira na misitu ya asili.

 
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea Hifadhi ya Amani 
 
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kulia akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu wakati wa ziara yake ya siku moja 

NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayanu humo 
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akisistiza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo 
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sakale katika kata Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Muheza wakati wa ziara ya Naibu.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...